Monday, 13 March 2017

LIGI YA MABINGWA AFRIKA: YANGA NA ZANACO NGOMA DRAW


Young Africans (Yanga) imeshikwa shati na Zanaco ya Zambia kwa mabao 1-1...

Ulikuwa mchezo wa kwanza wa hatua ya 32.

Sasa Yanga inahitaji ushindi kama inataka kuingia kwenye makundi kutokana na Zanaco kuwa na bao la ugenini...

Mpaka tunaenda mapumziko Yanga ilikuwa inaongoza 1-0 na bao hilo lilipatikana mnamo dakika ya 39 kutoka kwa Simon Happygod Msuva.

Msuva aliweza kuwachambua mabeki wa Zanaco alipopotea pande kutoka kwa Mzambia Justin Zulu.

Attram Kwame anayetokea Ghana alifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 78.

Mabeki wa Yanga walikuwa wameduwaa wanasubiri Fair Play baada ya Obrey Chirwa kufanyiwa ndivyo sivyo lakini Zanaco waliendelea na hatimaye Kwame alitingisha nyavu...

No comments:

Post a Comment