Monday 28 August 2017

VODACOM PREMIER LEAGUE: YOUNG AFRICANS (YANGA) NGOMA DRAW NA LIPULI MECHI YA KWANZA YA LIGI


Young Africans (Yanga) imeanza ligi kwa kutoka sare ya 1-1 na Lipuli FC ya Iringa ndani ya Uwanja wa Uhuru...
Mabao hayo hayakupishana kwani bao la kwanza lilitoka kwa mchezaji wa zamani wa Azam FC Seif Abdallah Karihe mnamo dakika ya 44 na baada ya hapo dakika ya 45 Donald Ngoma ya Yanga alisawazisha...

Heka heka za bao la yanga zilitokana na kona safi kutoka kwa beki wa kulia Juma Abdul ambayo ilimkuta Ngoma na nyavu zitatingishwa...

Kikosi cha Lipuli kilikuwa na Agathon Mkwando, Asante Kwasi, Samuel Mathayo, Paul Ngalema, Novaty Lufunga, Omega Seme, Seif Abdallah, Shaban Zuberi, Ramadhan Madebe, Jerome Lambele, Malimi busungu na Musa Nampaka...

Kikosi cha Young Africans (Yanga) kilikuwa na Youthe Rostande, Juma Abdul, Gabriel Michael, Andrew 'Dante' Vincent, Kevin Yondan, Papy Kamabma Tshishimbi, Emmanuel Martin, Yussuf Mhilu, thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Ajib na Raphael Daudi.

No comments:

Post a Comment