Wednesday 23 August 2017

SIMBA SPORTS CLUB: KING KIBADEN | SIMBA HALL OF FAME

(Picha: Imani Kajula

Abdallah 'King' Kibaden ni mchezaji pekee aliyewahi kuichapa Yanga mabao 3 katika mechi moja...
Alipiga hat-trick mwaka 1977 katika mechi kati ya watani wa jadi Young Africans (Yanga) na Simba Sports Club wana wa Msimbazi...

Katika mechi hiyo Simba walishinda 6-0 na mabao 3 yalikuwa ya King Kibaden...

Simba walikuwa chini ya Dimiltier Samsarov kipindi hicho...King kibaden alisema "siku tatu kabla ya mchezo huo, Yanga ilikuwa na mechi tulitoka kambini na kwenda kuiangalia, Yanga ilishinda

"Kitendo cha Yanga kushinda, baada ya mechi mashabiki wao walitupiiga na maganda ya machungwa huku wakutuzomea kuwa tujiandae kwa kipigo.

"Vurugu za mashabiki wa yanga zilituumiza mno, tulipofika kambini, tuliingia uwanjani na kuanza kujifua ilikuwa tayari saa mbili usiku, tuliapa kulipa kisasi kwa kushinda mechi ya Jumamosi.


No comments:

Post a Comment