Sunday, 8 January 2017

MAPINDUZI CUP: AZAM FC (4G) YAILAZA YOUNG AFRICANS (YANGA) 4-0 NDANI YA UWANJA WA AMAAN


Azam walifanikiwa kumaliza juu ya kundi lao la B kwa kuwachapa Young Africans mabao 4 kwa 0 ndani ya uwanja wa Amaan huko Zanzibar...
Timu zote 2 zimemaliza wakiwa sare kwa pointi 7 lakini Azam wanaongoza kwa mabao ya kufunga....Katika Nusu Fainali Azam itacheza na mshindi ya 2 na Yanga itacheza na mshindi wa kwanza katika kundi hilo la B...John 'Adebayor' R. ,Bocco nahodha wa Azam ndio aliyefungulia dimba la mabao kipindi cha kwanza mapema sana kwenye dakika ya 2...Bao hili lilitokana na kiundo Joseph Maundi kupiga shuti kali na kipa Deo Munishi 'Dida' kupangua ndipo nahodha alipoona nafasi akatandika shuti kali na kutingisha nyavu...Young Africans (Yanga) hawakufanya sana mashambulizi tofauti na mechi za awali...Mabao mengine kipindi cha 2 yalitoka kwa Ghanaian international Yahya Mohammed dakika ya 54 kupitia kichwa...Mahundi dakika ya 80...Na bao la mwisho dakika ya 85 kutoka kwa Ghanaian international, Enock Atta Agyei, mwingine aliyetokea bench.

No comments:

Post a Comment