Thursday, 6 April 2017

YOUNG AFRICANS (YANGA): WACHEZAJI WAAMBIWA WAWE WAPOLE KATIKA HIKI KIPINDI KIGUMU


Wachezaji wa Young Africans watishia kugoma kutokana na masuala ya mishahara yao...


Katibu wa Yanga Boniface Mkwasa awataka wachezaji wawe wavumilivu katika kipindi kigumu wakati mambo yao yanafanyiwa kazi...Kuna michakato inafanyika ikiwemo harambee ili wachezaji walipwe haki zao...

Wachezaji hao wametishia kugoma kwenye mechi ya kimataifa itakayofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya MC Alger...

Ni mara ya kwanza mwaka huu Yanga kufikiria kugoma kutokana na madai yao.