Monday, 3 April 2017

VODACOM PREMIER LEAGUE: KAGERA SUGAR WAMLAZA MYAMA SIMBA 2-1


Mnyama wa Msimbazi Simba Sports Club jana ilianguka kwa Kagera Sugar huko Bukoba...


Kagera Sugar ilishinda mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2-1 ndani ya Uwanja wa Kaitaba jijini Bukoba...

Kijana Mbaraka Yusuf ndio aliyefungulia mabao mnamo dakika ya 27 kwa shuti kali pembeni ya box na kumwacha kipa DAniel Agyai akishindwa kufanya lolote...Mchezaji wa Simba wa zamani Christopher Edwards alipachika la 2...Kipindi cha 2 Simba walisaka sana bao na mnamo dakika ya 65 Yassin aliweza kuipatia Simba bao...


Kwa msimamo wa sasa wa ligi Kagera Sugar imepanda na kuwa wa 3 kwenye ligi huku Simba wamebakia nafasi ya 2 wakiwa na pointi 55...

Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 56 na matokeo haya yameiweka Simba katika hali ya kufukuzia nafasi ya kwanza.