Showing posts with label Ugaidi. Show all posts
Showing posts with label Ugaidi. Show all posts

Monday, 14 March 2016

TURKEY: BABA WA MCHEZAJI NYOTA WA GALATASARAY AFARIKI KWENYE BOMU HUKO ANKARA


Mchezaji maarufu huko Uturuki, Umut Balut, amepoteza baba mzazi, Kamel Bulut, kwenye bomu lililolipuka jijini Ankara jana jioni...Watu 37 wamepoteza maisha jana wakati watu wanarudi majumbani mwao na wengine wanaendelea na shughuli zao za kilasiku...


Mambo ya kigaidi yameikumba Uturuki kwa muda mrefu na sasa raia wa kawaida wanapoteza maisha bila sababu...Hali bado sio shwari katika mji mkuu huo wa Uturuki...



Marafiki, ndugu na jamaa walifika nyumbani kwa Umut kumpa pole katika kipindi hiki kigumu sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 14 November 2015

FRANCE: FRANCE YASHINDA MECHI DHIDI YA GERMANY HUKU WAKUSHAMBULIWA MABOMU


Ufaransa jana ilivamiwa na magaidi huku watu 120 wakipoteza maisha...


Hali ilikuwa mbaya sana jana usiku kwani katikati ya game ya Franza na Germany mabomu mawili walilipuka hukju rais wa nchi hiyo, Francois Hollande,  akiwa ndani ya uwanja akiangalia game...


Ilibidi wamtoe haraka rais na watu waingie uwanjani mpaka usalama wao uhakikiwe...Watu watatu walipoteza maisha eneo la uwanja...France ilishinda game hiyo lakini ilikumbwa na hali ya hatari ndani ya jiji la Paris ambako sehemu nyingine zilishambuliwa na wengine kushikiliwa mateka...


Ufaransa sasa imefunga mipaka yake yote na kutangaza hali ya hatari na jeshi lote liko kazini sasa...Wengi waliofariki walikuwa wanasikiliza mziki wa bendi moja ya kimarekani ya rock inayoitwa 'Eagle of Death Metal'...Tunawaombea kwa Mola wote waliopatwa na mkasa huu...Bofya hapa upate habari zaidi.