Showing posts with label Jerome Valcke. Show all posts
Showing posts with label Jerome Valcke. Show all posts

Saturday, 14 May 2016

FIFA: MWANAMKE WA KWANZA ACHAGULIWA NAFASI YA JUU FIFA


FIFA kwa mara ya kwanza wamechagua mwanamke kushika nafasi ya juu sana...Fatma Samba Diouf Samoura atakuwa Karibu Mkuu wa FIFA kuanzia June...Samoura anatokea Umoja wa Mataifa (UN) ambako amefanya kazi kwa miaka mingi...Rais wa FIFA Infantino amesema FIFA inadhamira ya kubadilika na kutokana na dhamira hiyo wamechukua mtu wa nje kabisa...Samoura yanachukua nafasi ya Jerome Valcke ambae amesimamishwa kutokana na tuhuma za rushwa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 14 January 2016

FIFA: KATIBU MKUU WA FIFA ATIMULIWA

 
Jerome Valcke

Jerome Valcke ametimuliwa na Shirikisho la Soka Duniani Fifa...Valcke amefukuzwa kutokana na kuhusika na mambo ya rushwa ambayo pia yanahusu kufaidika kwa uuzaji wa ticket za World Cup...Valcke ambae ni mfaransa mwenye umri wa miaka 55 amekanusha kuhusika lakini kwa sasa kazi imeota mabawa na Dr. Marcus Kattner atakaimu nafasi hiyo...
 
Markus Katttner, Kaimu Katibu Mkuu FIFA

Pamoja na mengineyo anahusika na matumizi mabaya ya pesa ya Fifa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 8 October 2015

FIFA: BLATTER NA PLATINI WASIMAMISHWA



Kamati ya nidhamu imewasimamisha Sepp Blatter, Michel Platini na Jerome Valcke kwa muda wa siku 90...Blatter ni rais wa FIFA, Platini ni makamu rais na Valcke ni katibu na wamesimamishwa kutokana na contract ambayo haikuisaidia FIFA na pia pesa kiasi cha milioni 1.32 pounds za Uingereza alizopokea Platini kutoka kwa Blatter...FIFA pia wamemsimamisha makamu rais wa zamani Chung-Mong joon miaka 6... 


Issa Hayatou ambaye ni rais wa CAF atakuwa rais wa muda wa FIFA na amesema hato ingia kwenye kinyanganyiro cha kutafuta rais mpya wa FIFA...Bofya hapa upate habari zaidi.