Showing posts with label Rome Masters. Show all posts
Showing posts with label Rome Masters. Show all posts

Tuesday, 10 May 2016

CHARITY TENNIS MATCH: KIFAA HATARI CHA ROMA FRANCESCO TOTTI NA BAD BOY WA AUSTRALIA


Mmoja kati ya wachezaji wakali sana wa Italy Francesco Totti na mkali wa tennis kutoka Australia na namba 20 duniani  Nick Kyrgios kijana hatari wa tennis ambae ana mbwembwe nyingi sana akiwa kwenye court walikutana na kucheza mechi ya kirafiki ya tennis doubles ili kusaidia wasio jiweza...


Mechi hiyo ya Charity ilifanyika Rome ambako mashindano ya ATP ya Rome Masters karibu yanaanza...


Kwa Waitaliano Totti ni mchezaji bora kuliko wote maada amecheza mechi zaidi ya 600 kwa nchi yake na ameshinda tuzi nyingi sana za ndani na nje ya Italy...


Kwa sasa Totti anaichezea Roma na bado hajasema kama ataendelea kwani umri umesogea sana sasa...Bofya hapa upate habari zaidi

Tuesday, 3 May 2016

MADRID OPEN: FEDERER AMEJITOA KWA SABABU YA MAUMIVU YA MGONGO


Roger Federer ameamua kutoka kwenye mashindano ya Madrid Open baada ya kuumiza mgongo Jumamosi akiwa anafanya mazoezi...Hali ikiendelea poa atacheza Masters ya Rome kuanzia tarehe 9 May mpaka 15...Kwa sasa Federer ni namba 3 duniani...Bofya hapa upate habari zaidi.