Thursday, 19 January 2017

VODACOM PREMIER LEAGUE: MBEYA CITY NA AZAM FC NGOMA DRAW


Mbeya City waliwakomalia matajiri wa Chamazi na mabingwa wa Mapinduzi Cup Azam FC na kutoka sare ya 0-0 ndani ya uwanja wa Azam Complex huko Chamazi Dar es Salaam...
Azam sasa wana pointi 31 kati ya mechi 19...Wako nafasi ya 3 sasa chini ya Young Africans Sports Club (Yanga)...Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 45...Mechi kwa ujumla ilikuwa nzuri na ya kupimana sana lakini kipindi cha kwanza Mbeya City walijihami kiaina...Mchezaji mpya wa Mbeya City, Mrisho Khalfan Ngassa, aliingizwa kipindi cha 2 na kuwa hatari sana katika lango la Azam na hatimaye kufanikiwa kugonga mwamba.

No comments:

Post a Comment