Sunday, 29 January 2017

SIMBA SPORTS CLUB: HANS POPPE ASEMA HAWATAINGIA KICHWA KICHWA KWA OKWI


Mwenyekiti wa Usajili wa Club ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema siala la Emmanuel Okwi litajadiliwa kwa kina na hawataingia kicha kichwa kumsajili Okwi...
Simba inabidi wajiridhishe sana na kiwango cha Okwi kabla hajasajiliwa tena kwenye club hiyo ya msimbazi..."Okwi ni mchezaji wetu na Simba ni nyumbani kwake. Milango iko wazi kwake kurejea, lakini litapofukia suala la kusajiliwa tena, lazima kamati ya ufundi ijiridhishe kuhusu kiwango chake" Alisema Hans Pope akiongea na Bin Zubeiry Sports-Online...


Okwi hivi karibunui timu yake ya SonderjyskE ilivunja mkataba wake kwa makubaliano ya hiari kati yake na timu hiyo...Okwi ambae pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes, na pia aliwahi kuichezea Sports Club Villa kabla ya kuja kuichezea Simba...Timu nyingine aliyewahi kuichezea ni Etoile du Sahel...

No comments:

Post a Comment