Sunday, 31 May 2015

FA CUP: ARSENAL YAWEKA REKODI KWA KUSHINDA TENA KOMBE LA FA


Arsenal wameshinda kombe kongwe la FA ndani ya uwanja wa Wembley jana...Arsenal waliwachapa Aston Villa 4-0 bila ubishi katika game kali sana jana jioni...Mpira waliocheza Arsenal ulikuwa wa kiwango cha juu sana mwanzo mwisho na kufanikiwa kupata mabao 4 ya akili...


Rekodi ya jana ya Arsenal ni ya vikombe 12 vya FA...Arsenal imekuwa timu yenye vikombe vingi vya kuliko timu yeyote...Kombe hilo lilikabidhiwa na Prince William mjukuu wa kwanza wa Malkia...Prince William ni mshabiki wa timu ya Villa..Bofya hapa upate habari zaidi.

FIFA: SEPP BLATTER ASHANGAZA WATU KWA USHINDI


Sepp Blatter ameshangaza wadau wa soka duniani kwa kuchaguiwa kuwa rais wa shirikisho la soka duniani Fifa...Blatter alifanikiwa kushinda uchaguzi ambao ulikuwa wa watu 2 na mwenzake Prince Ali wa Jordan aliamua kukubali matokeo.Blater alipata kura 133 dhidi ya kura 73 za Prince Ali kwenye round ya kwanza...Mshangao unakuja kutokana na wakuu kadhaa kukamatwa na kufunguliwa mashtka na nchi ya Marekani na sasa wanasubiri kujibu mashtaka hayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 29 May 2015

EPL: SOUTHAMPTON WAKATAA DAU LA LIVERPOOL


Southampton wametupa mbali ombi la Liverpool la kumnyakua beki wa kulia Nathaniel Clyne kwa pounds milioni 10...Liverpool wataruditena na dau jipya kwa kuwa beki wao Glen Johnson anamalizia mkataba wake hivi karibuni...Nathaniel Clyne mwenye umri wa miaka 24 alitoka Crystal Palace kabla ya kuingia Southampton July 2012...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 28 May 2015

FIFA: UEFA WATAKA UCHAGUZI WA RAIS UHAIRISHWE


Wa kuu wa mpira wa Ulaya wanakutana leo ili kujadili jinsi ya kushawishi wenzao kwamba uchaguzi wa rais wa Fifa usifanyike kutokana na kukamatwa kwa viongozi wa juu kutokana na rushwa...Wakuu wa Uefa wanasema kukamatwa kwa viongovi kunaonyesha jinsi gani rushwa ilivyokomaa ndani ya Fifa...Uefa wanasisitiza mabadiliko ya uongozi ndani ya Fifa na pia uchaguzi ufanyike baada ya miezi 6...Bofya hapa upate habari zaidi. 

Wednesday, 27 May 2015

FIFA: MAKAMU MWENYEKITI WA FIFA NA WENGINE 5 WAKAMATWA


Jeffrey Webb Makamu Mwenyekiti wa Fifa na wengine 5 wamekamatwa na polisi kuhusiana na rushwa na kusafisha pesa haramu...Wamekamatwa wakiwa ndani ya  hoteli ya nyota 5 ya Baur au Lac mjini Zurich, Uswisi wakiwa wanajiandaa na uchaguzi mkuu wa Fifa Ijumaa ijayo...Polisi walivamia hiyo hoteli bila kumshtua mtu na kuwakamata hao maofisa na baada ya hapo wafanyakazi wa hoteli walianza kuchanganyikiwa wakiwa hawajui cha kufanya...

Jeff Webb.
Inasemekana polisi waliombwa na polisi wa Marekani kutokana na uchunguzi wa muda mrefu...Watuhumiwa wanasubiri wasafirishwe kwenda Marekani kujibu mashtaka hayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 26 May 2015

REAL MADRID: RAPHAEL BENITEZ MBIONI KUTUA MADRID


Kocha wa zamani wa Liverpool Raphael Benitez karibu ataingia Real Madrid msimu wake ukiisha Napoli Jumapili ijayo...Benitez bado haja saini mkataba lakini mazungumzo yako mbali sana...Carlo Ancelotti alifukuzwa na meneja wa Real Madrid baada ya kukaa hapo Bernabeu miaka 2...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 25 May 2015

F1: TOTO WOLFF AMWOMBA RADHI LEWIS HAMILTON


Toto Wolff boss na mmiliki wa 30% Mercedes 
Mercedes kupitia boss Toto Wolff amemwomba radhi Lewis Hamilton baada ya team ya Mercedes kuchemsha masesabu yaliyofanya Hamilton ashindwe kushinda Monaco GP....Wolf amesema anaomba msmaha na hilo kosa litashughulikiwa...

Lewis akitoa gari tayari kwa mashindanio
(Getty Images)
Hamilton hakulaumu timu ya yake ya Mercedes lakin ialikasirika sana na kusema haisumbui atajaribu tena...Bofya hapa uate habari zaidi.

Sunday, 24 May 2015

VOLLEYBALL: MECK SADIKI CUP TAYARI KUANZA MAY 28


Kwa mara ya 2 sasa kombe la volleyball la Meck Sadiki (Jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa sasa) liko tayari kuanza May 28 mpaka May 31...Kombe la Meck Sadik limetayarishwa na Chama cha Volleyball Dar es Salaam (DAREVA)...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 23 May 2015

F1: LEWIS HAMILTON KWA MARA YA KWANZA ATAANZA MBELE MONACO GP


Lewis Hamilton ataanza mbele kabisa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya F1...Hamilton alimpita mwenzake Nico Rosgerg kwa sekunde 0.342...Sebastian Vettel wa Ferrari akichukua nafasi ya 3 na Ricciardo wa Red Bull nafasi ya 4...Hamilton amefurahi sana na kusema imechukua muda mrefu sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

NBA: THE NBA LEAGUE IS A LEAGUE WITH THE MOST PAYOUT


NBA is a league that on an average the players get paid $4.6 million in the 2014-15 season.
 

Friday, 22 May 2015

FIFA: LUIS FIGO AJITOA KWENYE MBIO ZA KUWANIA URAIS


Luis Figo ameamua kujitoa kwenye mbio za kuwania urais wa Fifa....Figo alijitoa siku moja na Michael Van Praag na kumwacha Sepp Blatter kupamba na mtu mmoja ambae ni Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan...


Blatter bado ananafasi kubwa ya kuwa rais wa Fifa kwa mara ya 5...Member association 209 zote nina kura ya kumchagua rais wa Fifa na Michael Van Praag amesema atamsupport Prince wa Jordan...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 21 May 2015

EPL: SUNDERLAND YAPONEA CHUPUCHUPU


Sunderland jana usiku waliponea chupuchupu kushuka daraja katika game yao dhidi ya Arsenal ndani ya Emirates....Mechi iliisha 0-0 na kuifanya Sunderland kubakia kwenye ligi ya wakali wa wakali kwa mwaka wa 9 sasa...Sunderland wamshukuru sana kipa wao Costel Plantilimon kwa kuzuia mabao kibao hasa dakika za mwisho...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: LEWIS HAMILTON KUBAKIA MERCEDES


Lewis Hamilton atendelea kubakia team Mercedes kwa miaka 3 ijayo tofauti na uvumi kwamba anahamia team ya Ferrari...Lewis ametia saini mkataba wa kubakia Mercedes ambapo atapokea pounds milioni 27 kwa mwaka kwa miaka 3...Lewis amesema amefurhi kubakia Mercedes na pia gari analoendesha sasa ni bora kuliko yote ya nyuma...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday, 20 May 2015

LIVERPOOL F.C.: RAHEEM STERLING AZOMEWA


Raheem Sterling alizomewa jana kwenye tuzo za wanasoka bora wa club ya Liverpool...Sterling alizomewa kutokana na kutaka kuondoka club ya Livepool kwasababu anataka dau kubwa...Raheem alizomewa wakati anapokea tuzo ya mwanasoka bora kijana wa mwaka wa Liverpool...Wakati wanaonyesha mabao yake kwenye luninga watu walikaa kimya tofauti na mabao ya Coutinho watu walikuwa wakishangilia...Dogo Raheem alipata wakati mgumu sana wakati anatoa salam za kuwashukuru wachezaji wenzake...Bofya hapa upate habari zaidi.


COSAFA CUP: TANZANIA LAZIMA WASHINDE LEO

Mart Nooij (Backpagepix)
Tanzania na Lesotho lazima washinde mechi zao leo au wanarudi nyumbani...Tanzania ilichapwa mechi yake ya kwanza...Timu zote zilishangaza wadau kwa kufungwa mechi zao za kwanza...Lesotho walichapwa na Madagascar 2-1 na Tanzania ambao walicheza vizuri na kushambulia sana walizubaa na kuchapwa 1-0...Leo lazima timu hizi zifanye kweli bila uzembe kama wanataka kubaki kwenye michuano...Bofya hapa upate habari zaidi.

INDIANAPOLIS 500: JAMES HINCHCLIFFE AFANYIWA UPASUAJI BAADA YA AJALI MBAYA


James Hinchcliffe wa timu ya Schmidt Peterson Motorsports anayetokea nchi ya Canada amepata ajali mbaya kwenye Indy 500 baada ya kugonga ukuta akiwa spidi na gari kuwaka moto...James alikimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa haraka...Hali yake inaendelea vizuri lakini bado yuko Intensive Care...


Hii ni ajali ya 4 mbaya kwenye Indy 500 ndani ya wiki na hii ni baada ya kubadilisha sheria kufanya gari zisikimbie sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 19 May 2015

EPL: CHELSEA HOI KWA WEST BROMWICH ALBION


Chelsea jana walikuwa kituko kwani walikuwa kama watoto watukutu ambao sio mabingwa kabisa...Chelsea walichapwa 3 na West Bromwich Albion bila ubishi...Kipindi cha kwanza kwenye dakika takriban ya 27 kulitokea mzozo kati ya Costa na McAuley na Costa akalambishwa kadi ya njano...Wakati wachezaji wengi wanajadiliana na refa Cesc Fabregas alipiga mpira ukamgonga Brunt...Fabregas akalambishwa kadi nyekundu...


Mourinho nae alisema eti sababu ya kufungwa ni timu kubwa zimewaachia Chelsea wachukue ubingwa mapema...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: RATIBA YA MECHI ZINAZOKUJA (GMT)

WED 20 MAY 2015 - PREMIER LEAGUE
  • ArsenalvSunderland19:45
SUN 24 MAY 2015 - PREMIER LEAGUE
  • ArsenalvWest Brom15:00
  • Aston VillavBurnley15:00
  • ChelseavSunderland15:00
  • Crystal PalacevSwansea15:00
  • EvertonvTottenham15:00
  • HullvMan Utd15:00
  • LeicestervQPR15:00
  • Man CityvSouthampton15:00
  • NewcastlevWest Ham15:00
  • StokevLiverpool15:00

Monday, 18 May 2015

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
No movement1Chelsea364284
No movement2Man City374376
No movement3Arsenal363271
No movement4Man Utd372569
No movement5Liverpool37962
No movement6Tottenham37461
No movement7Southampton372360
No movement8Swansea37-256
No movement9Stoke37-251
No movement10Everton37-147
No movement11West Ham37-147
No movement12Crystal Palace37-545
No movement13West Brom36-1341
No movement14Leicester37-1338
No movement15Aston Villa37-2538
No movement16Sunderland36-2037
No movement17Newcastle37-2536
No movement18Hull37-1834
No movement19Burnley37-2630
No movement20QPR37-2730