Tuesday, 24 January 2017

DANISH SUPERLIGA: EMMANUEL OKWI ATEMWA NA CLUB YA SONDERJYSKE HUKO DENMARK


Timu ya ligi kuu ya Denmark SonderjyskE imesitisha mkataba na mchezaji Emmanuel Okwi...Okwi ambae ni striker wa Uganda Cranes amecheza mechi chache sana na timu hiyo ya ligi ya Superliga ndani ya miaka 2...Timu hiyo na Okwi walikubaliana mkataba usitishwe kwa manufaa ya wote wawili,  club na mchezaji...Okwi amewahi kuzichezea timu kubwa za Tanzania, Young Africans (Yanga) na Simba Sports Club,  na pia amewahi kuzichezea timu za Etoile du Sahel ya Tunisia na Sports Club Villa ya Uganda...Kuna tetesi Simba wanataka kumtumia tena...Kuna mshabiki matata sana wa Simba Kassim Mwandoro ambae tukimpata huyo atatuelezea kama tetesi hizi ni za kweli au la. 

No comments:

Post a Comment