Showing posts with label Riadha. Show all posts
Showing posts with label Riadha. Show all posts

Tuesday, 12 July 2016

KIGALI PEACE MARATHON 2016: MDAU WA MAX SPORTS FRANSIS KASSIDI NA UTORE LEMA NA WADAU WENGINE WALITUWAKILISHA KIGALI MARATHON


Wadau wakubwa wa Max Sports wakiongozwa na mdau Fransis Kassidi walituwakilisha Kigali Peace Marathon 2016 nchini Rwanda...


Wadau walikuwa wako fit kabisa na walijitahidi sana huku wakifanya networking na wadau wengine wa kinyarwanda...


Safi sana wadau kwa kutuwakilisha huko Kigali...Wengi tuigeni mfano wa hawa wadau...

Wednesday, 6 July 2016

SOUTH AFRICA: OSCAR PISTORIUS AFUNGWA MIAKA 6


Mwanariadha mlemavu kutoka Africa ya Kusini, Oscar Pistorius, amefungwa miaka 6...Oscar amefungwa baada ya mahakama kusikiliza tena kesi yake ya kumuua rafiki yake wa kike...Mwanasheria wa Oscar amesema wamekubali hukumu hiyo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 29 April 2016

REGIONAL U-20 ATHLETICS CHAMPIONSHIP: VIJANA KUCHUANA UWANJA WA TAIFA KUANZIA LEO


Mashindano ya riadha ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 yameanza leo Uwanja wa Taifa...Mashindano haya ni yakikanda na ni muhimu sana kwani wanariadha wanaweza kufuzu kwenda kwenye mashindano ya kimataifa ya IAAF Junior Championship Bydgoszcz nchini Poland kuanzia July 19 mpaka July 24...Nchi ambazo zitashiriki ni Djibouti, Rwanda, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan ya Kusini, Uganda, Sudan na Zanzibar...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 14 March 2016

ATHLETICS: WAYDE VAN NIEKERK KUTOKA AFRIKA YA KUSINI AWEKA REKODI MPYA KATIKA RIADHA


Wayde van Niekerk amekuwa mtu wa kwanza kukimbia chini ya sekunde 10 kwenye mita 100, sekunde 20 mita 200 na sekunde 44mita 400...Van Niekerk alitumia sekunde 9.98 katika mbio za mita 100  huko Bloemfontein ukijumlisha na sekunde 90.94 mita 200 na sekunde 43.48 mita 400 taji la dunia...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 10 March 2016

ATHLETICS: SEAN SAFO-ANTWI ARUHUSIWA KUBEBA BENDERA YA GHANA


Mwanariadha kwenye asili ya Ghana, Sean Safo-Antwi, anayekimbia kutumia bendera ya Uingereza ameamua kurudi na kupeperusha bendera ya Ghana...

Wednesday, 25 November 2015

ATHLETICS: MAKAO MAKUU YA RIADHA KENYA YAZINGIRWA NA WANARIADHA



Ofisi kuu ya riadha ya nchini Kenya imezungukwa na wanariadha ilikuzuia maafisa wa kuingia ofisini...Habari kutoka Kenya zinasema wanaridha hao wanataka maafisa kujiuzulu kutokana na kashfa inayowakabili viongozi hao...Pia wamelaumu kuwa viongozi hao wameshindwa kutatua suala la kutumia madawa ya kuongeza nguvu...Wanariadha hao wanataka uongozi uendeshwe na wanariadha wa zamani wanaojua masuala ya riadha...Bofya hapa upate habari zaidi.
 

Saturday, 29 August 2015

2015 WORLD ATHLETICS CHAMPIONSHIP: BOLT AIBEBA TENA JAMAICA KWENYE 4×100


Usain Bolt ameisaidia Jamaica kuchukua medani ya dhahabu kwenye michuano mikali ya dunia ya riadha huko China...Bolt alishinda kwa muda wa 37.36 muda mzuri kabisa na alimpita Justin Gatlin wa timu ya Marekani ambayo ilikataliwa nafasi ya 2 baada ya kukosea kupokezana kijiti...Nasafi ya 2 ilichukuliwa na China na nafasi ya 3 ilienda kwa Canada...Bofya hapa upate habari zaidi.