Thursday, 9 March 2017

LIGI YA MABINGWA AFRIKA: KIINGILIO CHA MECHI YA YANGA NA ZANACO KITAKUWA 3,000


Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Zanaco ya Zambia na Young Africans (Yanga) ya Dar es Salaam itafanyika Jumamosi...
Mechi hiyo itakuwa na kiingilio cha 3,000...Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa viingilio vitakuwa kama ifuatavyo...VIP A 20,000, VIP B na C ni 15,000 na wengine wote 3,000...

Mechi itarushwa 'live' na Azam TV kuwapa fursa watanzania wengine waweze kuangalia mechi...Yanga imeshaingia kambini tayari kujifua na kujiweka tayari karika mechi ya timu 32 zilizobakia...

Kocha George Lwandamina atakutana na timu yake tena lakini atakuwa upande mwingine wa uwanja akiisaidia Yanga kupata ushindi.

No comments:

Post a Comment