Tuesday, 20 January 2015

AFCON 2015: GHANA CHALI KWA SENEGAL


Ghana imeshindwa kushikilia draw baada ya kuchapwa 2-1 na Senegal...Kweli mpira dakika zote maana substitute Moussa Sow alifunga bao la 2 mwishoni kabisa pembeni ya box na kuwapa Simba wa Teranga ushindi muhimu sana...Ghana walianza kufunga baada ya winger wa Everton Christian Astu kufanyiwa foul na aliyefunga bao alikuwa Andrew Ayew...

Ayew akishangilia bao la 1
Baada ya hapo Senegal walipambana na Kara Mbodj aliwakosakosa Ghana kwa kugonga mwamba na dabae stiker wa Stoke City Mame Biram Diof alisawazisha...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 19 January 2015

EPL: ARSENAL YAICHAPA MAN CITY BILA UBISHI


Arsenal imewanyamazisha watu waliokuwa wanaibeza baada ya kuichapa Manchester City 2-0 ndani ya Etihad...Game ilikuwa kali sana na timu zote zilikuwa makini kushambulia na kuzuia mabao lakini City walikuwa wana pwaya sana na labda Aguero ndiye aliyejituma kupita wenzake...Carzola alifunga bao la kwanza la penalty baada ya Kompany kumfanyia ndivyo sivyo Monreal ndani ya 18...


Arsenal walibadilisha style yao na kuweka mkazo kwenye defense na kupunguza ile kasi yao ya kawaida ya kushambulia kama nyuki...Bao la 2 lilitoka kwa Giroud dakika ya 67 baada ya kumtoka beki kiaina na kupachika bao...Bofya hapa upate habari zaidi.

AFCON 2015: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

SUN 18 JAN 2015 - AFRICA CUP OF NATIONS

Sunday, 18 January 2015

ITF/CAT EAST AFRICA JUNIOR TOURNAMENT: MTANZANIA AIBUKA MSHINDI


Mandi Juma mtanzania kijana ameiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia ya tennis baada ya kushinda michuano ya kimataifa ya Afrika Mashriki jijini Dar es Salaam...

VPL: RUVU YAPONEA CHUPUCHUPU


Yanga na Ruvu Shoting walitoka 0-0 katika mechi kali ambayo Yanga ilionyesha uwezo wa hali ya juu...Ruvu nao walikuwa wabishi na kukosa nafasi nyingi za wazi walizo tengeneza...Pamoja na timu zote kucheza vizuri kulikuwa na foul nyingi kwenye game na mwamuzi alikuwa yuko busy kusuluhisha masuala ya ndivyo sivyo...Katika mechi ya awali Ruvu walichapwa 7-0 na Yanga na sasa wamekomaa hawataki tena kuaibishwa...Bofya hapa upate habari zaidi.

AFCON 2015: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

AFCON 2015: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

SAT 17 JAN 2015 - AFRICA CUP OF NATIONS

Saturday, 17 January 2015

EPL: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

TAIFA STARS: NOOIJ ATAJA KIKOSI CHA KUIKABILI RWANDA


Kikosi cha watu 26 kimetajwa na kocha Mart Nooij wa Taifa Stars tayari kupambana na Rwanda kwenye mechi ya kirafiki...Mechi hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 22 January jiji Mwanza ndani ya CCM Kirumba...Taifa Stars watakuwa kambini kuanzia leo jijini Dar na wengine 10 wataanza kujifua leo huko Mwanza...Nooij amechagua kikosi kutokana na umwi na pia anaangalia michuano ya African Nations Chamionship (CHAN) mwaka huu...Bofya hapa uate habai zaidi.

Friday, 16 January 2015

EPL: DEFOE AMALIZA TARATIBU ZA USAJILI SUNDERLAND


Jermain Defoe amemaliza usajili wake na timu ya Sunderland leo baada ya kubadilishana na Jozy Altidore ambaye anaenda Toronto FC...Defoe ameingia Sunderland kwa mkataba wa pound milioni 3.5...Defoe anategemea kucheza kwenye mechi kesho dhidi ya timu yake ya zamani Tottenham Hotspur...Bofya hapa upate habari zaidi.

COPA DEL REY: TORRES AISIMAMISHA REAL MADRID


Fernando Torres anaendelea kufanya vizuri na timu yake ya Atletico Madrid na jana amefunga mabao 2 dhidi ya Real Madrid...Bao la 1 mwanzo kabisa kipindi cha 1 na bao lingine mwanzo kabisa kipindi cha 2...Mechi iliisha 2-2 lakini Atletiko walikuwa tayari wana advantage ya mabao 2 mechi ya awali kwahiyo wameita kwa aggragate ya 4-2...Bofya hapa upate habari zaidi.

FIFA: DAVID GINOLA KUJITOSA MBIO ZA URAIS


France international wa zamani David Ginola ameamua anataka kuongoza Fifa...Atapambana na Sepp Blatter kuwania urais wa chama cha mpira duniani...Kuwania urais wa Fifa inahitaji kupata support ya vyama vikubwa 5 vya mpira na pia uwe unajihusisha na mrira kwa miaka 2 kati ya miaka 5...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND (GMT)

SAT 17 JAN 2015 - PREMIER LEAGUE
  • Aston VillavLiverpool15:00
  • BurnleyvCrystal Palace15:00
  • LeicestervStoke15:00
  • QPRvMan Utd15:00
  • SwanseavChelsea15:00
  • TottenhamvSunderland15:00
  • NewcastlevSouthampton17:30
SUN 18 JAN 2015 - PREMIER LEAGUE
  • West HamvHull13:30
  • Man CityvArsenal16:00

Thursday, 15 January 2015

EPL: FLETCHER MBIONI KUONDOKA


Darren Flecther Scottish international anataka kuondoka Manchester United na Tony Pulis wa West Brom anamtaka...Mkataba wake unaisha na katika dirisha dogo la usajili timu nyingi zinamtaka baada ya kusikia kapona matatizo yake ya tumbo...Fletcher alishkuwa kaimu captain chini ya Van Gaal lakini alianza mechi chache hususan kama 5 hivi...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday, 14 January 2015

ITF/CAT EASTERN AFRICA JUNIOR CHAMPIONSHIP 2015: TANZANIA YAFANYA VIZURI


Vijana wa Tanzania waendelea kuinyanyua bendrya ya taifa juu kwenye michuano mikali ya vijana ya tennis katika viwanja vya Gymkhana Club jijini Dar Es Salaam...Deogratius Felix wa Tanzania  alimchapa Kael Shah kutoka Kenya 1-6 6-1 6-4...Vijana wote hao walionyesha tennis ya hali ya kimataifa na kweli Afrika Mashariki tuna vipaji safi ni juhudi zetu binafsi kuvikuza...Mandi JF nae kwa upande wa kina dada U-14 amejitahidi sana na kuingia fainali ya michuano hiyo...Endelea kufuatilia matokea hapa hapa Max Sports...

NFL: JETS WAPATA KOCHA MPYA


New York Jets yapata kocha mpya ambae anajaza nafasi ya Rex Ryan ambae amekuwa kocha wa Buffalo Bills...Kocha mpya ni Todd Bowles ambae alikuwa coordinator wa Arizona Cardinals...Bowles anaingia Jets baada ya masaa 4 kutangazwa general manager mpya Mike Maccagnan...Jets wanajaribu kujipanga upya baada ya kufanya vibaya sana na kuwa na record ya 4-12...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: FALCAO ANAWEZA AKAONDOKA MAN UNITED


Radamel Falcao anaweza akaondoka Manchester United na kuchezea timu nyingine kubwa...Habari hizi zimetolewa na agent wake kutokana na uhalisi kuwa Falcao ameshindwa kuvuma Manchester United...Falcao toka aingie amefunga mabao 3 tu na alikuwa kwa mkopo wa milioni 6 na kama United wanamtaka inabidi watoe milioni 40 pounds na inavyoonekana Man United hawakotayari kutoa mpunga wote huo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 13 January 2015

RACING KINGS: A TANZANIAN HAS WON IN BRAZIL


Tanzania has made its mark in Brazil after winning a track & field race. 
 

FASDO TANZANIA: KOMBE LA VIJANA 2015


Wadau vijana wa soka nchini mnakaribishwa kujiunga kombe la vijana la Fasdo Tanzania 2015...Pata habari zaidi hapo juu...Tukuze vipaji vya vijana wetu...

BALLON D'OR: CRISTIANO RONALDO MCHEZAJI BORA DUNIANI


Cristiano Ronaldo amechaguliwa tena kwa mara ya 2 mfululizo kuwa mchezaji bora wa dunia...Ronaldo amewashinda forward wa Barcelona Lionel Messi na kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer...Kwa upande wa wanawake Nadine Kessler wa Wolfsburg na pia anaichezea timu yake ya Germany amenyakua ushindi...Goli la mwaka limeenda kwa James Rodriguez na kocha wa mwaka amekuwa Joachim Low aliyewapeleka Germany fainali ya World Cup...Kocha wa mwaka kwa upade wa mpira wa wanawake ni kocha wa Wolfsburg Ralf Kellermann...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 12 January 2015

NFL: COLTS YAISHANGAZA BRONCOS


Denver Broncos wamechapwa 24-13 na Indianapolis Colts kitu ambacho hawakutegemea...Denver kabla ya game walikuwa na record ya game 8-0 na wastani wa points 35 kwa mechi lakini Andrew Luck aliwanyamazisha kwa touchdown passes 2 na kumpita Payton Manning na timu yake...Sasa Colts watakutana na wakali New England Patriots (13-4)...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL:MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
No movement1Chelsea212749
No movement2Man City212547
Moving up3Southampton212039
Moving down4Man Utd211337
Moving up5Arsenal211236
Moving down6Tottenham21134
No movement7West Ham21733
No movement8Liverpool21232
No movement9Swansea21130
No movement10Newcastle21-827
No movement11Stoke21-526
No movement12Everton21-422
No movement13Aston Villa21-1222
No movement14West Brom21-921
No movement15Crystal Palace21-920
No movement16Sunderland21-1320
No movement17Burnley21-1420
No movement18Hull21-719
No movement19QPR21-1419
No movement20Leicester21-1317

LA LIGA: MESSI ASEMA HAENDI POPOTE


Lionel Messi ameamua kumaliza mino'gono ambayo ilikuwa imeiwekea kiwingu timu yake ya Barcelona...Messi amesema haendi poote si Chelsea wala Manchester City na hajaomba club imfukuze mtu...Messi alisema hayo baada ya game kali dhidi ya Atletico Madrid ambayo Barca walishinda 3-1...Tetesi ziliibuka baada ya kutoelewana kwa kocha Enrique na star huyo na sasa issue iko wazi Messi bado yupo yupo...Bofya hapa upate habari zaidi.