Showing posts with label Mandi Furaji. Show all posts
Showing posts with label Mandi Furaji. Show all posts

Thursday, 7 January 2016

EAST AFRICA JUNIOR TENNIS CHAMPIONSHIP 2016: OMAR SULLE NA MANDI FURAJI KUONGOZA KUNDI LA VIJANA 10 KWENYE MICHUANO MIKALI YA TENNIS

Omar Sulle
Michuano ya East Africa Junior Championship ambayo yatafanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 9 mpaka 17 kwa upande wa Tanzania yataongozwa na vijana Omar Sulle na Mandi Furaji...Vijana hawa wanauzoefu wa michuano ya kimataifa na wataongoza wenzao 10 ambao watashiriki mashindano hayo makubwa...
 
Stephanie Mbaya
Kocha wao Nicholaus Jonas amesema vijana walichaguliwa kutokana na jinsi walivyo jitahidi katika michuano mbali mbali ya mwaka jana...Jonas amewataja vijana ambao wako kwenye timu ya Tanzania kuwa ni Faith Nnko, Neema Chakindo, Kanuti Alagwa, na Rajab Musa kwenye U-12...Wengine ni Esther Nankulanga, Jackline Kayuga, Deogratus Ernest na Yusuf Godwin kwenye U-14...

 
Mandi Juma Furaji

Mandi Furaja na Emiliana Tarimo watashiriki  kundi la U-14...Omar Sulle na Hassan Yambi watashiriki kundi la U-16...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 18 January 2015

ITF/CAT EAST AFRICA JUNIOR TOURNAMENT: MTANZANIA AIBUKA MSHINDI


Mandi Juma mtanzania kijana ameiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia ya tennis baada ya kushinda michuano ya kimataifa ya Afrika Mashriki jijini Dar es Salaam...