Showing posts with label Donald Ngoma. Show all posts
Showing posts with label Donald Ngoma. Show all posts

Wednesday, 4 May 2016

VPL: YANGA NJIA NYEUPE SASA


Dar es Salaam Young Africans au kwa jina maarufu Yanga wako nafasi nzuri ya kwa twaa ubingwa baada ya kushinda mechi yao dhidi ya Stand United huko uwanja wa Kambarage Shynyanga...Yanga walitupiamo magoli 3 na mabao mawili yalitoka kwa mkali Donald Ngoma na la 3 kutoka kwa Ammis Tambwe...Hali ilivo sasa ni kwamba Yanga wana points 68 na wako points 9 mbele ya Azam FC kwahiyo Yanga wakishinda mechi moja kati ya 3 zilizobaki ubingwa wao...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 21 February 2016

VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA YAIZAMISHA SIMBA 2-0


Donald Ngoma na Amis Tambwe ndio walioizamisha Simba katika mechi ya ligi iliyofanyika jijini Dar es Salaam...Watani wa jadi Simba na Yanga huwa ni gumzo kubwa hapa mjini na jana Yanga waliweza kuwanyamazisha watani kwa mabao 2...Kwa sasa Yanga wako kileleni wakiwa na points 46 na Simba wamekaa nafasi ya 3 baada ya Azam FC kushinda 3-0 dhidi ya Mbeya City...Simba na Azam wako sawa kwa points lakini Azam wako mbele kwa tofauti ya mabao...Yanga walikuwa na bahati wakati mchezaji wa Simba Abdi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kufanya foul mara 2...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 22 January 2016

VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA YAIRARUA MAJIMAJI 5-0


Yanga iko kilelelni baada ya kuirarua Maji Maji 5-0 bila ubishi...Yanga walianza mapema kupachika bao kupitia kwa Thabani Kamusoko dakika ya 4...Mpaka half-time ubao ulisoma 1-0 lakini baada ya kuingia kipindi cha 2 tu Donald Ngoma alipokwa pasi kutoka kwa Kamusoko na hakufanya kosa...Nyota wa mchezo alikuwa Amis Tambwe ambae aliondoka na hat-trick safi na sasa ni mfungaji bora kwenye ligi...Katika mechi nyingine kali Mwadui waliwachapa Kagera Sugar 2-1...Bofya hapa upate habari zaidi.