Showing posts with label Daniel Sturridge. Show all posts
Showing posts with label Daniel Sturridge. Show all posts

Thursday, 18 July 2019

Wednesday, 1 June 2016

EURO 2016: RASHFORD NDANI YA SQUAD YA ENGLAND


Marcus Rashford ameitwa ndani ya timu ya Taifa ya England...Roy Hodghson ametaja timu yake ya wachezaji 23 wataoingia Euro 2016 nchini France...Daniel Sturridge wa Liverpool nae ndani ya squad ya England...Drinkwater na Andros Townsend wameachwa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 19 May 2016

EUROPA LEAGUE FINALS: SEVILLA MABINGWA TENA


Sevilla wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa League kwa kuwatandika Liverpool 3-1 jana usiku huko Basel...Liverpool walianza kucheza vizuri na hatimaye kabla ya mapumziko walipata bao safi kabisa kupitia Daniel Sturridge...Sturridge ni mchezaji wa kwanza kufunga bao Europa League/UEFA Cup toka Robbie Fowler afungee mwaka 2001...


Kipindi cha 2 Sevilla sijui waliambiwa nini na kocha maana walibadilisha game na kucheza kwa akili nyingi...Liverpool wakaanza kuchanganyikiwa na badae Klopp akamtoa Lallana lakini haikusaidia kwani Sevilla walikuwa wanacheza vizuri zaidi...


Katika mipira 4 iliyolenga goli mipira 3 ya Sevilla imeingia nyavuni...Wafungani wa Sevilla walikuwa Kevin Gameiro dakika ya 46 na Andujar Moreno mabao 2 dakika ya 64 na 70...


Sevilla wamefunga Sevilla wanachukua kombe kwa mara ya 3 mfululizo sasa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 6 May 2016

EUROPA 2016: LIVERPOOL FC YAINGIA FAINALI


Liverpool imefanikiwa kumtoa Villarreal kazi ambayo haikuwa rahisi lakini ndio hivyo tena wametinga fainali...Liverpool walishinda mabao 3-0 na aggregate ya 3-1...Liverpool waliingia wakiwa chini aggregate ya bao 1 lakini Bruno Soriano alijifunga na waka sawa 1-1 kwa aggregate...Bao la 2 ilitoka kwa Daniel Sturridge dakika ya 63 na bao la 3 lilitoka kwa Adam Lalana...Roberto Firmino alisaidia sana mabao yote kupatikana...Mabingwa watetezi Sevilla watakutana na Liverpool kwenye fainali ndani ya jiji la Basel tarehe 18 May...Sevilla waliwachapa Shakhtar Donetsk mabao 3-1 na aggregate ya 5-3...


Mshindi wa kombe la Europa anapata nafasi ya kucheza moja kwa moja Champions League na kwa Liverpool hatakama wako chini wakishinda watakuwa ndani ya Champions League...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 2 December 2013