Wednesday, 21 June 2017

YOUNG AFRICANS: RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ATUMA SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWANACHAMA NA MKEREKETWA MKUBWA WA YOUNG AFRICANS (YANGA) MAARUFU KWA JINA LA ALLY YANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, ametuma salam za rambirambi kwa wanafamilia na klabu ya Young Africans (Yanga) kwa msiba wa mwanachama na mkereketwa mkuwa wa klabu hiyo Mohammed 'Ally Yanga' Ally...
"Nimeguswa sana na kifo cha Ally Yanga, nilikuwa nae wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo alitoa mchango mkubwa wa uhamasishaji wa wananchi kukipigia kura chama changu cha CCM, na pia amekua akiongoza mashabiki wenzake kuishabikia timu ya Yanga na timu ya taifa bila kuchoka, kwa kweli alikuwa hodari sana katika ushabiki wake." alisema Rais Magufuli.

Ally Yanga alipata ajali ya gari huko Mpwapwa mkoa wa Dodoma wakati wa mbio za Mwenge...

Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipongolo...Ally Yanga alifarika hapo hapo...

Ally enzi za uhai wake alikuwa akikonga mioyo ya mashabiki wa Yanga kwa kujipaka masizi usoni na kuweka matambara tumboni aonekane anakitambi pamoja na miwani mikubwa sana ya kijani...

Wadau wa Yanga walikuwa wanamuita Ally Tumbo Tumbo au Ally Masizi...

Mazishi ya Ally Yanga yatafanyika leo...Msiba uko Shinyanga maeneo ya stendi ya zamani...

Pumzika kwa amani Ally Yanga.