Wednesday, 17 May 2017

YOUNG AFRICANS: DAU LA UDHAMINI LA SPORTPESA KWA YANGA KUBWA KULIKO LA SIMBA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga,
akipeana mkono na Mtendaji Mkuu SportPesa Pavel Slavkov 

Yanga imepata dau kubwa kuliko watani wao wa jadi Simba Sports Club kwenye udhamini mpya kutoka kampuni kubwa ya SportPesa...
Yanga imesaini mkataba na SportPesa wa miaka 5 kwa dau la Bilioni 5...

Simba wao pia walisaini mkataba na SportPresa ka dau la Bilioni 4.96...

Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Ndugu Tarimba Abbas, amesema SportPesa imesaini na yanga kwa malengo ya kuendeleza soka ilifie malengo ya klabu hiyo...

Pia amesema hizo pesa zitatolewa kwa awamu...Awamu ya kwanza zitatolewa shilingi milioni 950...

Pesa hizio inabidi badae zithibitishwe matumizi yake na pia matumizi yake yawe ya kuendeleza soka...

Motisha zingine zitakuwepo endapo watafanya vizuri...Kwa mfano watapewa milioni 100 wakishinda Ligi Kuu Tanzania Bara...

"Pia ikishinda michuano kama Kagame pia watapewa zawadi na wakufanya vuzuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika watapata zawadi ya Milioni 250." alisema Tarimba...

Yanga na Simba watapewa jezi zenye chata ya SportPesa pamoja na vifaa vingine vingi tu.