Monday, 22 May 2017

TANZANIA FOOTBALL FEDERATION (TFF) : RAIS WA TFF JAMAL MALINZI ASEMA ABDULRAHMAN MUSSA NA SIMON MSUVA KUZAWADIWA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Jamal Malinzi amesema wafungaji bora Abdulrahman Mussa na Simon Msuva wote watapata zawadi...
Mussa anatokea Ruvu Shooting Stars na Msuva anatokea Young Africans (Yanga)...

Malinzi akiwa Libreville ambako alikuwa na timu ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 alisema wachezaji hao wawili watapata nusu ya milioni 5.8 ...

Mussa na Msuva wote walimaliza Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na mabao 14 kila mmoja...

"Kwa kuwa vijana wetu Abdulrahman Mussa na Simon Msuva wamefungana kwa mabao katika Ligi Kuu (kila mmoja 14), wote ni wafungaji bora na watapewa zawadi sawa (kutoka) Sh. Milioni 5.8." alisema Malinzi.