Tuesday, 16 May 2017

SIMBA SPORTS CLUB: MO KUKAA CHINI NA UONGOZI WA SIMBA LEOMohammed 'MO' Dewji atakaa chini na uongozi wa Simba Sports Club kujaribu kumalizana matatizo yao toka SportPesa wachukue udhamini wa klabu hiyo...
Ni kikao kinachofuatia kikao cha suluhu juzi baina ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zakaria Hans Poppe na Kamati ya Utendaji chini ya Rais Evens Elieza Aveva...

Hans Poppe alijiuzulu Kamati ya Utendaji ambapo pia kwa maana hiyo amejivua Uenyekiti wa Kamati ya Usajili na pia Kamati ya Ujenzi wa Bunju Complex...

Hans Poppe alichukizwa kutohusishwa katika mkataba baina ya SportPesa na Simba Sports Club...


MO Dewji pia alikasirika pia kwamba hakuhusishwa na mkataba wa Simba na SportsPesa...MO ni mwekezaji mzawa ambae alitaka kunua hisa nyingi kwenye klabu ya Simba...MO anadai alipwe fidia zake ambazo zinafikia Bilioni 1.4...Fidia hiyo ni pesa alizokuwa akiikopesha Simba ili waweze kulipia benchi la ufundi na mishahara ya wachezaji...Ilikuwa milioni 80 kila mwezi..