Friday, 19 May 2017

SERENGETI BOYS: SERENGETI BOYS WAKO FITI SANA NA WAINYUKA ANGOLA MABA0 2-1


Serengeti Boys wameonyesha mpira wa hali ya juu sana baada ya kuwachapa Angola 2-1 katika kundi lao la B ambapo sasa wanaongoza kundi hilo...
Vijana hao wamekosa mabao mengi sana kwani kasi yao ilikuwa nzuri sana ila hakukuwa na wamaliziaji...

Naftali aliwanyanyua mashabiki mnamo dakika 6 tu za mchezo huo alipotingisha nyavu kwa kichwa...Alipokea krosi kutoka kwa Enrick Vitalis....Angola waliweza kusawazisha dakika ya 16 kupitia Pedro...

Abdul Suleiman mnamo dakika ya 68 aliwapa raha sana watanzania alipopachika bao safi ambalo lilitokana na pasi safi kutoka kwa Yohana Oscar Mkomola...Mpira huo ulichezwa ndani ya Uwanja wa L'Amittee jijini Libreville, Gabon...

Serengeti sasa wana pointi 4 katika kundi lao la B...

Mechi ya mwisho kwa Serengeti Boys kwenye kundi B itafanyika Mei 21 dhidi ya Niger.