Monday, 22 May 2017

CAF U-17 CHAMPIONSHIP 2017: SERENGETI BOYS WATOLEWA KIFUA MBELE WAKIWA MASHUJAA


Serengeti Boys wametolewa kwenye michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17...
Serengeti Boys jana ilikuwa uwanjani Port Gentil na Niger na kuchapwa 1-0...

Kwa upande mwingine vijana wa Tanzania walicheza mpira wa kiwango cha juu sana lakini umaliziaji ulikuwa hafifu...

Niger waikuwa nawanacheza rafu sana na kujigarazagaza sana ili wapoteze muda...

Niger walipata bao ambalo lilikuwa linaonekana off-side na pia kipa hakuufuata ipasavyo...Refa akapeta na kuuweka mpira kati...

Kiwango cha mpira cha Serengeti kilikuwa kikubwa sana kuliko Niger na pia kuliko timu zote walizochezanazo...

Mpira ni dakika 90 na tuombee waendelee kujianda na michuano mingine ya badae.