Sunday, 2 April 2017

VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA KILELENI TENA


Young Africans (Yanga) wamerejea tena kileleni baada ya kuwachapa wanalambalamba au matajiri wa Chamazi Azam FC 1-0...

Haruna Niyonzima alivuta moja ndefu iliyomkuta Mzambia Obrey Chirwa ambae alimtoka beki wa Azam FC Yakubu Mohammed na kupachika bao dakika ya 70...Yanga ulipata pigo kubwa mnamo dakika ya 30 baada ya kiungo tegemezi, Justin Zulu, kuumizwa vibaya mguu wa kushoto na kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin ambae ni winga...

Kiungo Himidi Mao wa Azam FC ndio aliosababisha Zulu aumie baada ya kumwekeia mguu wakati Zulu anataka kupiga mpira...Mchezo huo mkali ilichezeshwa na refa wa kike mwenye beji ya FIFA Deonesya anayetokea Kagera...

Yanga sasa inashikilia uskani wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 56 wakiwa wamecheza mechi 25...Simba Sports Club wako nafasi ya 2.