Sunday, 23 April 2017

TANZANIA FOOTBALL FEDERATION: SIMBA SPORTS CLUB YAPOKONYWA POINTI 3


Simba Sports Club imetolewa poiti 3 na Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (Tanzania Football Federation - TFF)...


Simba walipewa pointi hizo baada ya kulalamikia mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ndani ya Uwanja wa Kaitaba huko Bukoba...

Selestine Mwesigwa, Katibu wa TFF, amesema leo akiwa ofisi za TFF kwamba Kamati imegundua mapungufu ya uamuzi wa Kamati ya Saa 72...

Alisema kwanza Simba hawakuwakilisha malalamiko yao ndani ya muda uliotakiwa chini ya kanuni ya 20 kifungu cha kwanza