Sunday, 23 April 2017

SIMBA SPORTS CLUB: AVEVA ATAKA SIMBA WAANDAMANE TAREHE 25 APRILI


Mwenyekiti wa Simba Sports Club, Evans Aveva, amemuandikia Kamanda wa Polisi Simon Siro ili Simba waweze kuwa na maandamano ya amani tarehe 25 Aprili...


Maandamano hayo ni ya kulalamaika juu ya uonevu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema Aveva...

Katika hiyo barua ambayo pia imenakiliwa kwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo inataka wanachama wote wa Simba kuandamana kutoka Makao Makuu ya Klabu ya Simba Msimbazi mpaka Wizara ya Habari...

Maandamano haya yanakuja baada ya TFF kumtaka msemaji mkuu wa Simba Sports Club Hajji Manara ajieleze kuhusu utovu wa nidhamu.