Thursday, 6 April 2017

SERENGETI BOYS: TIMU YA TAIFA YA VIJANA YA SERENGETI BOYS YASEPA KWENDA KUWEKA KAMBI MOROCCO


Timu ya Vijana ya Taifa ya Serengeti Boys iliondoka jijini Dar es Salaam tayari kuweka kambi rasmi nchini Morocco...


Serengeti Boys watakuwa Morocco kwa muda wa mwezi 1 wakijifua na kujiweka fiti kwa mechi za Kombe la Mataifa Afrika...Mechi hizo zitaanza Mei 14 nchini Gabon...

Serengeti walianza kambi hapa nyumbani January 29 na kucheza mechi za kujipima nguvu dhidi ya Burundi au kwa jina lingine maarufu "Intamba Murugamba" mara 2...Mara ya kwanza Serengeti walishinda 3-0 na mara ya 2 Serengeti walishinda 2-0 ndani ya Uwanja wa Kaitaba Bukoba...Pia walicheza na Ghana au "Black Starlets" na kutoka sare ya maba 2-2.