Thursday, 9 March 2017

YOUNG AFRICANS: YANGA YAFANYA MAUAJI HATARI YAICHAPA KILUVYA UNITED MABAO 6-1


Young Africans ni harati sana na bila huruma wameitandika Kiluvya United mabao 6-1 ndani ya Uwanja wa Jamhuri jijini Dar es Salaam...
Yanga sasa wamefanikiwa kuingia robo-fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania au kwa jina maarufu sana Azam Sports Federation Cup (ASFC)...

Obrey Chirwa ndiye aliyekuwa kinara kwa kupata mabao 4 na kupewa mpira aende nao nyumbani kwani ukifunga mabao 3 ni kitu wanaita hat-trick (mazingaombwe ya kwenye kofia) unaenda na mpira nyumbani kama kumbukumbu ya kufanya vizuri...

Yanga itakutana na Prisons kwenye robo-fainali ya kombe hilo la Azam Sports Federation Machi 18 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa..