Thursday, 23 March 2017

SIMBA SPORTS CLUB: METHOD MWANJALI YUKO FITI KUCHEZA SASA


Mzimbabwe Method Mwanjali ambae alikuwa nje kutokana na kuwa majeruhi sasa yuko fiti tayari kupambana...


Beki Kati huyo ni tegemezi wa Simba Sports Club na ni habari njema kwa timu na mashabiki...Mwanjali alikuwa na tatizo kwenye goti lake ambalo alipata majeraha hayo Februari 11 Simba wakicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons...

Mwanjali alikosa Kombe la Shirikisho au Azam Sports Federation Cup (ASFC)...Simba walishinda 3-0 huko Dodoma dhidi ya wenyeji Polisi jijini Dodoma na waliweza kuwachapa Madini FC bao 1 ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid na pia Mererani FC walichapwa bao 1.