Thursday, 2 March 2017

SERENGETI BOYS: WAZIRI WA MICHEZO MHE. NAPE NNAUYE ACHAGUA KAMATI YA HAMASA YA SERENGETI BOYS


Waziri wa michezo Mheshimiwa Nape Nnauye amechagua kamati ya kuihamasisha Serengeti Boys...
Nape alitangaza Kamati hiyo kwenye kongamani la kujadili juu ya ushiriki wa Tanzania katika mashindani ya kimataifa...Kamati hiyo itaongozwa na Mtangazaji maarufu sana Charles Hilary na itakuwa na wajumbe 10 tu...Katibu wa Kamati hiyo atakuwa Mwesigwa Selestine ambae ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)...Wajumbe wengine wa Kamaiti hiyo ni mtangazaji maarufu na mchoraji vibonzo al-maafu kama "Kipanya" ndugu Maulid Kitenge, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni kubwa ya simu za mkononi Airtel Beatrice Singano na Hoyace Temu ambae alikuwa Miss Tanzania mwaka 1999...Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Michezo Hassan Abbas nae yupo kwenye Kamati hiyo, Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo, Mkurugenzi wa Couds Media Ruge Mutahaba, Wansanii maarufu wa muziki Ali 'King' Kiba na Diamond Platinumz nao wamo kwenye kamati...