Friday, 31 March 2017

SERENGETI BOYS: SERENGETI BOYS WAICHAPA BURUNDI 3-0 NDANI YA KAITABA


Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 imewachapa Burundi 3-0 ndani ya uwanja wa Kaitaba jijini Bukoba...


Mchezo huo ulikuwa wa kirafiki na kusaidia Serengeti Boys kujinoa tayari kwa mashindano ya vijana Afrika mwezi Mei huko Gabon...

Serengeti Boys walikuwa makini sana safu ya nyuma na walikabili mashambulizi ya Burundi...Mechi ilikuwa ni kushambuliana kwa zame na mpaka wanaenda mapumzikoni Serengeti Boys ilikuwa juu maba0 2-0...


Wafungaji walikuwa kiungo Muhsin Makame mnamo dakika ya 19 na beki wa kushoto Nickson Kababage dakika ya 38...Nahodha Kevin Nashon Naftali alifunga bao la 3 kupitia tuta dakika ya 72 baada ya mchezaji wa Burundi kuunawa mpira ndani ya box.