Sunday, 26 March 2017

INTERNATIONAL FRIENDLY: MBWANA SAMATTA AIZAMISHA BOTSWANA


Nahotha wa Taifa Stars ameisaidia timu take kwa kupachika mabao yote mawili katika mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana ndani ya Uwanja wa Taifa...


Samatta alipachika mabao hayo moja kila kipindi... Bao la kwanza lolikuja mapema sana wakati beki ya Botswana imelala...Ibrahim Ajib alikuwa karibu aongeze bao katikato ya kipindi cha kwanza...


Kipindi cha pili Stars walianza kwa moto na Simon Msuva aliwakosakosa Botswana mabao mawili...

Samatta mnamo dakika ya 88 aliwika kwa kuipa Stars  bao la 2 kupitia free-kick hatari kabisa ambayo imimwacha kipa wa Botswana,  Kabelo Dambe, akiwa amesimama akitoa macho kwa mshangao mkubwa... 

Mechi ilihudhuriwa na Waziri mpya wa Michezo Mh. Harrison  Mwakyembe na Waziri wa zamani wa Michezo Mh. Nape Nnauye... Mh. Nape alishangiliwa sana wa umati wote uwanjani kutokana na mambo yaliotokea hivi karibuni.