Monday, 20 March 2017

AZAM SPORTS FEDERATION CUP: SIMBA YATINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA TFF


Simba Sports Club imeingia nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuichapa Madini FC bao 1 tu...


Laudit Mavugo ndie aliyesaidia kuipeleka Simba nusu fainali ya kombe hilo ambalo pia linajulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa bao ka kichwa mnamo dakika ya 55 baada ya mpira kumshinda beki wa Madini FC Hamisi Hamisi...

Mchezo huo ulikuwa unaushindani mkubwa ma ulichezewa ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume...Mnamo dakika ya 69 winga hatati Shiza Kichuya akiga shuti kali ambalo liliokolewa na beki Hamisi Hamisi...

Simba sasa itaungana na Mwadui FC ambao waliwatoa wenyeji Kagera Sugar kwa mabao 2-1...